Mkulima Library inatoa huduma zifuatazo:
- Kukusanya, kuweka pamoja na kutoa machapisho yenye habari na taarifa sahihi za kilimo.
- Kutoa nafasi kwa wakulima kujisomea ndani ya maktaba;
- Kutoa huduma za rejea pamoja na kujibu maswali mbalimbali;
- Kudurufu machapisho mbalimbali kwa wale wanaohitaji nakala;
- Kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya TEHAMA katika kujipatia taarifa mbalimbali za kilimo;
- Kutoa huduma za video za mafunzo mbalimbali ya kilimo kupitia mtandao wa YouTube
SNAL inaendelea kuboresha ghala la machapisho mbalimbali ya kielektroniki kwa ajili ya mahitaji ya wakulima walio mbali na maktaba. Huduma zote za kujisomea na kutumia Mkulima Library ni bure hadi pale msomaji atakapohitaji kudurufu chapisho atapaswa kuchangia gharama hizo.
Ni kwa jinsi gani huduma zinapatikana
Huduma za Mkulima Library kwa sasa zinapatikana kwa njia zifuatazo:
- Kutembelea moja kwa moja Maktaba ya Taifa ya Sokoine ya Kilimo - SNAL, SUA, kampasi kuu Morogoro.
- Kupitia kituo chetu cha Mkulima Library Youtube ambapo utaweza kuona video mbalimbali juu ya kilimo na fani zake.
Siku zijazo Mkulima Library mbali ya kupatikana kupitia mtandao huduma hizi zitapatikana kwenye maktaba zilizoko katika sehemu mbalimbali nchini.