Miongoni mwa njia za kuongeza na kukuza machapisho na taarifa mbalimbali ndani ya Maktaba yoyote ile, kupokea zawadi au msaada ni mojawapo ya njia kuu mbali ya ile ya kununua.
Hivi karibuni aliyekuwa mfanyakazi na mhadhiri mbobezi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Aida C.Isinika ambaye alikuwa katika Taasisi ya Elimu Endelevu (ICE) & CoEBS na ambaye amefanya kazi nyingi za ushauri katika sekta ya kilimo na maendeleo ameizawadia Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Sokoine (SNAL) vitabu vipatavyo 230 na hivyo kuongeza idadi ya machapisho katika maktaba hiyo.