Have any questions? +255 23 260 4639 snal@sua.ac.tz

Wakulima nchini Tanzania wamehimizwa kutumia Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Sokoine hususani kitengo cha Mkulima kilichopo maktaba ya Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

SNAL img 2

Hayo yamesemwa na ndugu Jabir A. Jabir ambaye ni mkutubi toka maktaba hiyo kwenye maonesho ya nanenane yaliyofanyika Agosti 2019, Morogoro. Ndugu Jabir alisema wakulima wa mazao, wafugaji wa mifugo, na wavuvi mbali mbali wanaweza kutembelea maktaba hiyo kwa kutumia njia ya kielektroniki au ana kwa ana. Aliongeza kuwa wahitaji wanaweza kutembelea Maktaba hiyo iliyopo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ili kupata majarida mbalimbali yatakayowawezesha kupata taarifa muhimu zitakazowasaidia kuboresha shughuli zao. Akifafanua njia rahisi ya kielekroniki inayoweza kutumika, alisema mkulima anaweza kutumia simu ya kiganjani (smartphone) na kutafuta tovuti ya Maktaba ya Taifa ya Kilimo ya Sokoine, kisha akabonyeza Mkulima kuingia kwenye tovuti ya kitengo cha mkulima baadae kubonyeza Mkulima au bonyeza hapa kutafuta machapisho ili kuingia moja kwa moja kwenye ukurasa wa ghala la machapisho. Aliongeza, kwenye ukurasa huo kuna sehemu ya kuandika kile unachotaka kutafuta, kwa mfano ufugaji kuku na kubonyeza nenda ili kupata majarida yaliyoandikwa kuhusu ufugaji wa kuku.

Sikiliza habari kamili


Bonyeza hapa kutafuta machapisho